Posts

Showing posts from 2018

LEO NAKULETEA HISTORIA YA MAISHA YA MICHAEL JACKSON

Image
Michel Jackson alizaliwa tarehe 29 August mwaka 1958, akiwa ni mtoto wa nane kati ya kumi wa mzee Joe Jackson na Catherine Jackson, alikuwa na madada wa 3 ambao ni Rebbie, La Toya na Janet, huku makaka zake ni Jackie, Tito, Jermaine, Marlon, Randy, na ndugu yake mwingine anayeitwa Brandon alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa. Alianza kuimba akiwa umri wa miaka mitano akiwa na kundi la Jackson 5, kundi lakifamilia kwani waimbaji wote katika kundi hilo walikuwa ni ndugu zake wa damu, kundi hilo lilifanya vizuri sana nchini marekani na dunia nzima kwa ujumla. Jackson hakuwa na mahusiano mazuri na baba yake Joe Joseph Jackson aliwahi kusema kuwa alikuwa na kawaida ya kumchapa Michael wakati akiwa mtoto, na Michael aliwahi kulalamika kuwa baba yake alikuwa akimnyanyasa kwa kumpiga hasa wakati wa Rehalse ingawa aliwahi kukiri kuwa baba yake alichangia kwa kiasi kikubwa yeye kupata mafanikio. 1968 Boby Taylor na The Vancouver waliligundua Kundi la Jackson 5 ambapo kundi hilo likasign...

NEW AUDIO KUTOKA KWA WASAFI #JIBEBE

Image
    Wasani kutoka lebo kubwa ya muziki Tanzania WCB wasafi wamekuja ngoma mpya kwa jina Jibebe kutoka kwenye nyimbo hiyo diamond platnumz mbosso pamoja na lavalava wakiwa wameshirikiana kufanya ngoma hiyo kuwa Kali nyimbo hi I imekuja baada ya collable ya diamond na harmonize kwangaru kufanya vizuri kwenye chati tofauti za mziki Afrika. Isikilize hapa https://youtu.be/0VIiM8csqc0

LEO KATIKA HISTORIA NAKULETEA MAISHA YA DIKTETA WA UGANDA IDD AMIN

Image
        Idi Amin Dada alikuwa mwanajeshi kutoka nchi ya Uganda aliyepindua serikali na kujifanya rais wa Uganda tangu mwaka 1971 hadi 1979 hadi alipofukuzwa na jeshi la Tanzania. Alitawala kidikteta ilhali uchumi wa nchi uliporomoka na makosa mengi ya jinai dhidi ya haki za kibinadamu zilitendwa. Idadi ya watu waliouawa Uganda kutokana na utawala wake imekadiriwa kuwa kati ya 100,000  na 500,000 Katika miaka yake ya kushika serikali Amin alibadilika kutoka uhusiano wa kirafiki na nchi za magharibi na hasa Israeli kuhamia upande wa Muammar Gaddafi wa Libya, Mobutu Sese Seko wa Zaire, Umoja wa Kisovyeti na Ujerumani ya Mashariki. Hata hivyo Amin alipata usaidizi wa ofisi ya upelelezi ya Marekani CIA iliyotuma silaha na vifaa vingine kwa jeshi lake. Mwaka 1977 Amin alivunja uhusiano wa kidiplomasia na Ufalme wa Maungano (Uingereza) akajitangaza kuwa alishinda na kujiongezea sifa ya CBE ("Conqueror of the British Empire"). Kuanzia wakati ule cheo chake...