Osama bin Mohammed bin Awad bin Laden alizaliwa Riyadh huko Saud Arabia katika famila ya ndugu Mohammed bin Awad bin Laden ambaye alikuwa ni tajiri mkubwa sana kwa nyakati hizo utajiri ambao aliupata kwa kazi yake ya ukandarasi, Osama bin Laden alizaliwa 10,march, 1957 kwa Hamida al-Attas alikuwa mke wa kumi katika orodha ya wake za baba yake Mohammed na ambaye alimpa taraka muda mfupi baada ya Osama kuzaliwa, Hivyo watoto aliozaliwa tumbo moja na Osama walikuwa jumla yao wanne akiwepo mwanamke mmoja ambaye ni dada yao. ELIMU Osama amehudhuria shule Al-Thager model school, na baadaye akahudhuria masomo ya Uchumi na biashara katika chuo cha KING ABDULAZIZ. Lakini pia alikuwa na shahada ya ufundi na ya maendeleo ya jamii. Ukweli ni kuwa alikuwa ni mtu aliyekuwa ni mtu mwenye bidii katika kila jambo au kazi, pamoja na hayo yote Osama aliipenda sana dini yake kupindukia kama walivyo waarabu wengine wenye itikadi kali, muda mwingi aliutumia kuichambua quran na kazi za kujitolea. Osama a...