LEO NAKULETEA HISTORIA YA MAISHA YA MICHAEL JACKSON
Michel Jackson alizaliwa tarehe 29 August mwaka 1958, akiwa ni mtoto wa nane kati ya kumi wa mzee Joe Jackson na Catherine Jackson, alikuwa na madada wa 3 ambao ni Rebbie, La Toya na Janet, huku makaka zake ni Jackie, Tito, Jermaine, Marlon, Randy, na ndugu yake mwingine anayeitwa Brandon alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa. Alianza kuimba akiwa umri wa miaka mitano akiwa na kundi la Jackson 5, kundi lakifamilia kwani waimbaji wote katika kundi hilo walikuwa ni ndugu zake wa damu, kundi hilo lilifanya vizuri sana nchini marekani na dunia nzima kwa ujumla. Jackson hakuwa na mahusiano mazuri na baba yake Joe Joseph Jackson aliwahi kusema kuwa alikuwa na kawaida ya kumchapa Michael wakati akiwa mtoto, na Michael aliwahi kulalamika kuwa baba yake alikuwa akimnyanyasa kwa kumpiga hasa wakati wa Rehalse ingawa aliwahi kukiri kuwa baba yake alichangia kwa kiasi kikubwa yeye kupata mafanikio. 1968 Boby Taylor na The Vancouver waliligundua Kundi la Jackson 5 ambapo kundi hilo likasign...
Comments
Post a Comment