MAJIBU YA MENEJA WA DIAMOND PLATNUMZ KWA ERIC SHIGONGO

Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kenye magazeti yako kw
a kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya...baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu  na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo instagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako... siku zote nimekuheshimu na Sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea Sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata...ili kesho ukawaambie vizuri waandishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana kama mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wwengine na watu mbalimbali.... tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu... Umekazana wiki nzima  kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond... ila sie tume kaa  kimya... na kujifanya unazunga eti unatushauri... kweli mtu unasema unampenda unamshauria instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?..... Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini? ...na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa  na wewe,  juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya @Harmonize_tz DARLIVE na tukakubaliana asilimia,  na hadi kupost tumepost... ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilikia na kutaka asilimia kuuuubwa wewe, eti sisi tuchukue  asilimia ndogo kabisa....tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya  juu ya kutaka asilimia kubwa...hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na amshabiki zao hii ndio kuwaeka  karibu wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe....mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na  kula Madawa....yote kutafuta sababu Msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato  Ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kum'bomoa msanii kupitia magazeti yako.....tafadhali heshimu heshima yetu kwakođź‘Ť...... "Mh Magufuli tafadhali Ulipo Kaza legeza, ona Wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoto vidogo vyao....

Comments

Popular posts from this blog

LEO NAKULETEA HISTORIA YA MAISHA YA MICHAEL JACKSON

LEO KATIKA HISTORIA NAKULETEA MAISHA YA SADDAM HUSSEIN

LEO KATIKA HISTORIA. KIFO CHA RAIS WA ZAMANI WA LIBYA MUAMMAR GADDAFI