Michel Jackson alizaliwa tarehe 29 August mwaka 1958, akiwa ni mtoto wa nane kati ya kumi wa mzee Joe Jackson na Catherine Jackson, alikuwa na madada wa 3 ambao ni Rebbie, La Toya na Janet, huku makaka zake ni Jackie, Tito, Jermaine, Marlon, Randy, na ndugu yake mwingine anayeitwa Brandon alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa. Alianza kuimba akiwa umri wa miaka mitano akiwa na kundi la Jackson 5, kundi lakifamilia kwani waimbaji wote katika kundi hilo walikuwa ni ndugu zake wa damu, kundi hilo lilifanya vizuri sana nchini marekani na dunia nzima kwa ujumla. Jackson hakuwa na mahusiano mazuri na baba yake Joe Joseph Jackson aliwahi kusema kuwa alikuwa na kawaida ya kumchapa Michael wakati akiwa mtoto, na Michael aliwahi kulalamika kuwa baba yake alikuwa akimnyanyasa kwa kumpiga hasa wakati wa Rehalse ingawa aliwahi kukiri kuwa baba yake alichangia kwa kiasi kikubwa yeye kupata mafanikio. 1968 Boby Taylor na The Vancouver waliligundua Kundi la Jackson 5 ambapo kundi hilo likasign...
Saddam Hussein akiwa kortini Alfajiri ya Jumamosi, 30 Desemba 2006 muda mfupi kabla ya saa 12:00, itakuwa siku ya kukumbukwa katika historia ya taifa la Iraq, kwa machungu au kwa furaha miongoni mwa wananchi wa taifa hilo kutokana na kunyongwa kwa aliyekuwa mtawala wa taifa hilo aliyeondolewa madarakani na majeshi ya kimataifa yakiongozwa na Marekani na Uingereza. Saddam Hussein Abd al-Majid al-Tikriti, ambaye alikuwa mtawala wa taifa la Iraq amekabiliwa na changamoto ya msemo huo kufuatia kutekelezwa kwa hukumu iliyotolewa na mahakama moja nchini Iraq ya ‘kunyongwa hadi kufa’ baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu wa kibinadamu uliomkabili licha ya kukata rufaa na ktupwa baadaye. Wengi tulizoea kusikia majina yake ya Saddam Hussein, lakini majina yake halisi ni kama yalivyotajwa hapo juu na alizaliwa tarehe 28, Aprili mwaka 1937 katika kijiji cha Tikrit katikati ya Iraq, na aliingia madarakani tarehe 16 Julai 1979 na kulitawala taifa hilo kwa ...
Wapiganaji dhidi ya Muammar Gaddafi wakionesha karavati ambalo kiongozi huyo alikuwa amejificha UTAWALA wa Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya umefikia kikomo jana baada ya kiongozi huyo kuuawa katika mapigano ya waasi ya miezi minane ya kuuondoa kumwondoa katika madaraka aliyokalia kwa miaka 42. Gaddafi alikufa kutokana na majeraha aliyoyapata jana katika mapigano hayo, yaliyosababisha kujeruhiwa vibaya katika miguu yake miwili, na kufariki dunia muda mfupi baadaye. Jinsi alivyouawa Kwa mujibu wa taarifa za viongozi wa Serikali ya Mpito Libya (NTC), kiongozi huyo alikufa jana baada ya kukamatwa katika mji wa Sirte alikozaliwa. Hata hivyo, habari za kuuawa kwake zilijaa na utata kutokana na kuelezwa mazingira tofauti. Mmoja wa walioshuhudia mauaji hayo, Bw. Abdel Majid Mlegta ambaye ni mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu wa NTC, katika mahojiano na Shirika la Habari la Uingereza (Reuters), alisema kuwa kiongozi huyo alikufa baada ya kupigwa risasi kichwani. "Gadda...
Comments
Post a Comment